Wednesday, 20 July 2016

Agizo la Makonda kuhusu waliovamia maeneo ya wazi Dar

 
 Na Kalonga Kasati

Ongezeko la idadi ya watu katika jiji la Dar es Salaam wanaokadiriwa kufikia milioni 10 limesababisha jiji kutokuwepo kwenye idadi ya majiji yenye mandhari nzuri ukilinganisha na majiji mengine Afrika na hata kwingineko duniani, baada ya wakazi wa jiji hilo kuvamia maeneo yaliyoachwa wazi na serikali.
Hali hiyo imemchochea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutamka kuwa huenda kwa miaka kumi ijayo maeneo ya wazi yakapotea ambapo amewaagiza madiwani wote katika mkoa huo kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja wanaratibu na kupata idadi kamili ya maeneo ya wazi yaliyopokwa ili waweze kuondoa watu katika maeneo hayo.


Hatua hiyo imefuata baada ya Paul Makonda kuteuliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kuwa mlezi wa vilabu vya soka mkoani humo, ambapo baada ya uteuzi huo chama hicho kilimwambia moja ya changamoto wanayokabiliana nayo ni upungufu wa viwanja vya michezo.

Mbali na kutumiwa kwenye michezo, pia Makonda ameeleza kuwa maeneo hayo yatakaporejeshwa yataweza kutumika pia kujengea shule na vituo na afya.


No comments:

Post a Comment