Monday, 6 June 2016
Polisi wametaja chanzo cha kifo cha Prince Nelson
Ripoti ya Polisi pamoja na uchunguzi wa Madaktari kutoka jimbo la Minnesota nchini Marekani umebaini kuwa mwanamuziki Prince Nelson, alifariki dunia kutokana na kuzidisha kiwango cha dawa.
Kwa mujibu wa madaktari waliofanya uchunguzi huo wa kifo cha mwanamuziki Prince, wanasema alizidisha kiwango cha dawa za kutuliza maumivu zijulikanazo kama Fentanyl. Dawa hizo zinadaiwa kuwa na nguvu mara hamsini zaidi ya dawa za kulevya za Heroin.
Hata hivyo dawa hizo hutumika wakati wa upasuaji na hasa wagonjwa ambao miili yao ni sugu kwa dawa nyingine za kutuliza maumivu.
Prince alikutwa amefariki dunia Aprili mwaka huu, ndani ya ‘lift’ katika makazi yake huko Minneapolis.
Siku moja kabla ya kifo chake inadaiwa kuwa alikuwa akihitaji msaada kutoka kwa daktari maalumu kutokana na maumivu ya mwili aliyokuwa akiyasikia. Hata hivyo polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kutokana na kifo hicho.
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment